Radio Mbiu 4.0.1

Radio Mbiu 4.0.1 4.1 and up Apk Free Download Updated Version

About this app:

Radio Mbiu- Sauti ya Faraja ni Radio ya kibiashara lakini inayofanya vipindi vyenye kuwanufaisha wasikilizaji kiroho na kimwili kwa pamoja, kuhabarisha na kuielimisha Jamii ya Watanzania kulingana na mazingira, rika na nyadhifa mbalimbali.
Radio Mbiu- Sauti ya Faraja inapatikana eneo la Bunena Wilaya ya Bukoba Mjini Mkoani Kagera na ofisi zake zinapatikana ndani ya viwanja vya Kanisa Mama la Jimbo Katoliki la Bukoba, ambalo ni Kigango cha Familia Takatifu.
Radio Mbiu-Sauti ya Faraja ni Nyumba ya Ukarimu kwa watu wote bila kujali rangi, dini, umri, kabila wala hali ya Mtu.
Radio Mbiu kwa sasa ina leseni ya hadhi Wilaya ambapo ina fursa ya kuwa na masafa matatu katika kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kubadilisha hadhi ya leseni ya sasa.
Lengo la kwanza katika mwaka huu wa kwanza ni kuhakikisha kuwa inasikika katika Mkoa wote wa Kagera kabla ya kujitanua na sehemu za mikoa ya karibu. Kwa sasa Radio Mbiu inasikika katika wilaya za Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini, Muleba, Karagwe, Misenyi, na baadhi ya maeneo ya wilaya za Kyerwa na Biharamulo. Eneo ambalo bado kufikiwa ni wilaya ya Ngara na baadhi ya maeneo ya wilaya za Kyerwa na Biharamulo.
...
Read more

App Information

VersionRatingAPP VoteSize
4.0.1 00-
RequirementUpdatedInstallsDeveloper
4.1 and upOctober 10, 2019500+WorldFamilyLab
High Speed Download